1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu

10 Mei 2012

Watu wenye ulemavu mara kwa mara katika maisha ya kila siku wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kubaguliwa.Wamekuwa wakitengwa na kukataliwa kutokana na ulemavu wao

https://p.dw.com/p/P2PE
Picha: LAIF

Pata nafasi ya kumfahamu mmoja wao, na kwa kupitia yeye utaifahamu dunia

Takriban asilimia kumi ya idadi ya watu wote duniani ni walemavu.Ingawaje wamekuwa wakijikimu maisha yao kwa kuombaomba katika miji barani Afrika, lakini madhila wanayokabiliana nayo walemavu hao ikiwa ni pamoja na wale wasiyoona yanapuuzwa.Baadhi ya walemavu wengine wamekuwa wakifungiwa majumbani na familia zao, kwasababu wanachukuliwa kama watazitia aibu familia hizo au hata kuwachukulia kuwa ni laana kutoka kwa mizimu.

Mikataba ipo ya kuwalinda walemavu.Hata hivyo idadi kubwa ya watu hao wameendelea kukumbana na vizuizi katika jamii.Wanatengwa katika maisha ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni, na mara kwa mara wamekuwa wakinyimwa haki za kushiriki katika siasa na kuwa huru kutoa fikra zao.

Kipindi hiki kipya cha mchezo wa radio´´ Learning by Ear Noa Bongo Jenga Maisha Yako kinatupeleka Maganye, mji wa kubuni uliyoko barani Afrika.Fuatilia hadithi ya Oluanda ambaye ghafla amejikuta mlemavu baada ya kukatwa mguu.Amejikuta akikabiliwa na changamoto mpya maishani.

Gundua ujumbe wake muhimu.Bila kujali iwapo mtu ni mlemavu au la, binaadamu wote ni sawa.Kila mtu ana ndoto na malengo na haki ya kutimiza ndoto na malengo hayo.

Kipindi cha Learning by Ear kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa,Kihausa, Kireno na Kiamharic.Kinafadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Ujerumani.