1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga kutumia Spray inayofutika haraka

9 Oktoba 2014

Kuanzia Oktoba 18, spray inayofutika haraka itaanza kutumika katika ligi za daraja tatu kuu za kandanda Ujerumani, wakati wa kupigwa mipira ya freekick. Maafisa wamesema hakuna sababu yoyote ya kutotumia spray hiyo

https://p.dw.com/p/1DSUu
Freistoßspray
Picha: picture-alliance/dpa

Baada ya utata kuzuka, hatimaye spray hiyo ya kufutika haraka itatumiwa katika Bundesliga, pamoja na ligi za divisheni ya pili na tatu, kuanzia Oktoba 18.

Refarii mkuu wa shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB Lutz Michael Fröhlich amesema masuala yote ya kisheria yametatuliwa na kila kitu kitakachohitajika ili kutekeleza matumizi ya spray hizo kimekamilika.

Kampuni inayokagua ubora wa bidhaa ya Ujerumani – TUEV iliifanyia vipimo spray hiyo wiki iliyopita na baadaye ikaripoti kuwa povu linalotumiwa siyo halali nchini Ujerumani au barani Ulaya kwa sababu ina kemikali zinazoathiri homoni za mwili. Pia TUEV ilisema kuwa spray hiyo inaweza kuwaka moto kwa urahisi, na ilhali mikebe yake haijawekwa alama au ishara ya kutahadharisha hilo. Lakini sasa vibandiko vimewekwa kwenye mikebe hiyo.

Fröhlich amesema kampuni inayouza spray hiyo imezingatia na kukagua kila kitu. Na sasa imeidhinishwa. Spray hiyo ilitumika kwa mafanikio wakati wa Kombe la Dunia na tayari inatumika katika ligi kadhaa za Ulaya ikiwa ni pamoja na England na Champions League.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Josephat Charo