1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Buhari anaongoza uchaguzi Nigeria

Admin.WagnerD30 Machi 2015

Matokeo ya uchaguzi nchini Nigeria, yanayotarajiwa kukaribiana sana , tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, yameanza kutolewa taratibu leo Jumatatu(30.03.2015) baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa juma

https://p.dw.com/p/1EzjG
Nigeria Bildergalerie Staatspräsidenten Muhammadu Buhari
Mgombea wa upinzani Mohammadu BuhariPicha: picture-alliance/AP Photo/A. Akinleye

Mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi huo nchini Nigeria Muhammadu Buhari anaonekana kuongoza na mapema kutokana na matokeo katika majimbo saba kati ya 36. Buhari amemshinda rais Jonathan katika sita kati ya majimbo saba ya kusini magharibi, kati na kaskazini, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi.

Nigeria Oppositionsführer Muhammadu Buhari in Kano
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Muhammadu BuhariPicha: DW

Chama cha upinzani cha All Progressives Congress APC hata hivyo kinapinga matokeo katika jimbo la River, makao makuu ya makampuni makubwa ya uchimbaji mafuta katika bara la Afrika, na kushutumu upigaji kura katika jimbo hilo na kuuita , "usiofaa na kichekesho".

Wanawake waandamana

Kiasi ya wanawake 2,000 waliokuwa wakiandamana kwa amani dhidi ya hatua za kupiga kura katika jimbo la River nchini humo wametawanywa kwa mabomu ya kutoa machozi leo(30.03.2015) na polisi wa kuzuwia ghasia, wakati wakijaribu kupeleka malalamiko yao kwa maafisa wa tume ya uchaguzi.

"Wakati tukiwa katika maandamano ya amani kuelekea ofisi za tume ya uchaguzi, tukitaka kuwafahamisha kwamba kulikuwa hakuna karatasi tza kupigia kura ama karatasi za matokeo , wanajeshi walianza kutushambilia kwa mabomu ya kutoa machozi na kutufukuza".

Baadhi ya wachunguzi wametoa sifa za tahadhari katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Wahl in Nigeria
Wananchi wakisubiria matokeo ya uchaguziPicha: Getty Images/Afp

Taasisi ya taifa nchini Marekani ya demokrasia , ambayo huhimiza demokrasia pamoja uwazi katika serikali , imeusifu uchaguzi huo, licha ya matatizo ya kiufundi pamoja na machafuko ya hapa na pale.

Marekani na Uingereza zaeleza wasi wasi wao

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Uingereza Philipp Hammond leo wameeleza wasi wasi wao kuhusu uwezekano wa kuingilia kati kisiasa katika zoezi la kuhesabu kura nchini Nigeria.

Wahl Nigeria Abuja
Vifaa vya kusoma kadi za wapiga kuraPicha: DW/Uwaisu A. Idris

"Hatujaona ushahidi wowote wa udanganyifu katika mchakato huu. Lakini kuna ishara zinazotia shaka katika zoezi zima la ukusanyaji wa mahesabu ya kura , ambapo kura hatimaye zinajumlishwa, huenda zoezi hilo likachafuliwa makusudi kwa kuingiliwa na wanasiasa," wamesema wanadiplomasia hao wawili katika taarifa ya pamoja.

Schweiz Lausanne Kerry Erklärung zu Iran Verhandlungen Atomstreit
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John KerryPicha: Reuters/B. Snyder

Uingereza na Marekani zimekaribisha , kura hiyo ambayo imeendeshwa "kwa kiasi kikubwa kwa amani", baada ya kurefushwa kwa siku mbili hadi Jumapili kutokana na kushindwa kufanyakazi kwa tekonolojia mpya iliyotayarishwa kusoma kadi za wapiga kura. Kadi hizo zimetayarishwa kupambana na udanganyifu katika uchaguzi.

Na huko katika majimbo ya Gombe na Bauchi kaskazini mashariki mwa Nigeria washukiwa wa kundi la Boko Haram wameuwawa leo katika mapigano , polisi na wakaazi wa eneo hilo wamesema.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre /

Mhariri: Mohammed Khelef