1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bach atetea maandalizi ya Michezo ya Rio 2016

2 Machi 2015

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach amesema bado ipo kazi nyingi ya kufanywa kabla ya Michezo ya Olimpiki mjini Rio kung'oa nanga mnamo Agosti 2016

https://p.dw.com/p/1Ejry
Thomas Bach Olympisches Komitee
Picha: picture alliance/epa/Jean-Christophe Bott

Bach hata hivyo ameonyesha matumaini kwa waandalizi wa mashindano hayo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini Brazil huku akisisitiza kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa mwendo unaofaa ili kuutayarisha mji huo kuandaa michezo hiyo kwa wakati unaofaa. "ni wazi kuwa, kamati ya maandalizi inastahili kuongeza mwendo wa matayarisho. Hatua zimepigwa ili kuvitayarisha viwanja. Lakini pia bado kuna kazi nyingi ya kufanywa na hakuna mda wa kupoteza. Hivyo tunajua ipo kazi ya kufanywa lakini tuna matumaini kuwa itafanyika".

Bach alikuwa mjini Rio mwishoni mwa wiki kwa ajili ya mkutano wa Bodi Kuu ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ambapo walijadili kuhusu mipango ya Michezo ya Rio pamoja na maswala mengine ya Olimpiki ikiwa ni pamoja na mashindano yatakayoandaliwa mjini Tokyo mwaka wa 2022. Tamasha la Olimpiki 2016 mjini Rio litakuwa la kwanza kuwahi kuandaliwa katika bara la Amerika ya Kusini.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef