1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alonso, Button kupeperusha bendera ya Ferrari

Admin.WagnerD12 Desemba 2014

Usiseme haiwezekani, huo ni msemo maarufu katika nyanja mbali mbali za maisha, na hata katika mbio za magari ya Formula one ambako Fernando Alonso ameamua kurejea katika magari ya McLaren

https://p.dw.com/p/1E3QU
McLaren-Honda Fernando Alonso British Jenson Button Präsentation 11.12.14
Picha: picture-alliance/Mclaren-Honda

Timu hiyo ya magari imetangaza wiki hii kwamba bingwa huyo mara mbili wa dunia wa Formula one ataendesha magari hayo msimu ujao pamoja na bingwa wa mwaka 2009 Jenson Button, kama ilivyotarajiwa miezi kadhaa iliyopita.

Lakini mwishoni mwa mwaka 2007, hatua kama hiyo ilikuwa inaonekana kama kichekesho tu. McLaren na Ferrari zilihusika katika kashfa ya upelelezi ambayo iliutikisa mchezo huo na MacLaren iliadhibiwa kwa kupigwa faini ya dola milioni 100 kwa kupata nyaraka za siri za kiufundi za Ferrari.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman