1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Kenya yafikia watu 228

5 Mei 2024

Mamlaka nchini Kenya zimesema kuwa idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko imeongezeka hadi kufikia watu 228.

https://p.dw.com/p/4fWXa
Mafuriko nchini Kenya yasababisha vifo vya zaidi ya watu 225
Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya wakiwa katika harakati za uokoaji kufuatia mafuriko : 22.04.2024Picha: Brian Inganga/AP/picture allinace

Tangu siku ya Jumamosi, watu tisa wameripotiwa kufariki huku jumla ya wengine 223,198 wakiathirika na mafuriko hayo.

Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura amesema wamewahamisha na kuwapeleka katika maeneo salama jumla ya watu 163,000. Siku ya Jumamosi, serikali mjini Nairobi ilitangaza mipango ya kupunguza athari za mafuriko hayo huku kukiwa na tahadhari ya Kimbunga Hidaya kupiga pwani za Kenya na Tanzania.

Soma pia: Ruto aahidi kuhamishwa wananchi ambao wamekubwa na mafuriko

Hata hivyo, mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania imetangaza leo kwamba kasi ya kimbunga Hidaya imedhoofika na si tishio tena kwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, tangu mwezi Machi, mvua kubwa na mafuriko vimesababisha uharibifu mkubwa katika nchini Kenya, Tanzania, Burundi, Somalia, Rwanda na maeneo mengine ya Afika Mashariki.